
Bernadette Zawadi, anayejulikana zaidi kwa jina la Rebo Queen, ni msanii anayekuja kwa kasi kutoka Nyarugusu, ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani.
Hivi karibuni, sauti inayodaiwa kuwa yake imevuja mitandaoni, ikimwonyesha akizungumza na mganga kutoka Nyarugusu, huku yeye akiwa bado anaishi Marekani. Katika sauti hiyo, inadaiwa Rebo Queen anazungumzia nia ya kumdhuru kwa njia za kishirikina msanii mwenzake anayefahamika kwa jina la Nazda.
Tukio hilo limeibua mjadala mkubwa mitandaoni, hasa ikizingatiwa kuwa Nazda anatarajiwa kuachia EP yake mpya siku ya Valentine Day, Februari 14, 2026. Mashabiki na wadau wa muziki wanaendelea kufuatilia kwa karibu kuona kitakachojiri, huku macho yakielekezwa zaidi kwenye kazi hiyo ijayo ya Nazda
ndao ya kijamii inaendelea kuchemka kufuatia sauti inayodaiwa kuvuja ikimhusu Rebo Queen, huku msanii Nazda akijiandaa kuachia EP yake mpya siku ya Valentine Day, Februari 14, 2026.
