Omriama is an online media platform delivering entertainment, music, business, and international news from Tanzania and around the world.

Wasanii wa Kibembe Wanaoendelea Kung’ara Marekani: ILUSTAR, JANY BOY na GASPER
GASPER / ILUSTAR/JANY BOY

Katika ulimwengu wa muziki na burudani unaoendelea kukua kwa kasi, wasanii wa jamii ya Wabembe wameanza kujitokeza na kuchukua nafasi kubwa kimataifa. Miongoni mwa majina yanayozidi kutajwa sana ni ILUSTAR, JANY BOY na GASPER — wasanii waliozaliwa Nyarugusu na kwa sasa wanaishi Marekani. Kupitia kazi zao, wamekuwa chachu ya matumaini na fahari kwa vijana wengi wa Kimbembe waliopo ndani na nje ya Afrika.

Kwa sasa, hawa watatu wameonekana kuwa wasanii pendwa wa Wabembe, hasa kutokana na matukio yao, maudhui wanayotoa, na namna wanavyopokelewa na mashabiki. Kila wanapotoa kazi mpya au kuonekana kwenye majukwaa ya burudani, mashabiki husubiri kwa hamu kubwa kuona nini kipya wanakuja nacho.

ILUSTAR

ILUSTAR – Mfalme wa Uchekeshaji kutoka Nyarugusu

ILUSTAR ni msanii mwenye vipaji vingi, hasa katika sekta ya uchekeshaji. Safari yake ilianza miaka ya nyuma, lakini mwaka 2024 hadi 2025 ndiyo imekuwa kipindi chake cha mafanikio makubwa zaidi. Ndani ya muda mfupi, ameweza kujijengea jina kubwa na kufikia hadhira ya kimataifa.

Kupitia mitandao ya kijamii, ILUSTAR ameweka rekodi ya kipekee:

TikTok: Wafuasi zaidi ya milioni 1.4 Instagram: Wafuasi zaidi ya 896,000

Mafanikio haya yamemfanya kuwa Mbembe wa kwanza kutoka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kufanikiwa na kutambulika duniani kote katika upande wa uchekeshaji.

Upande wa muziki, ILUSTAR pia amejaribu kuonesha kipaji chake kwa kutoa EP yake ya kwanza “DIZ WAY / DAZ WAY”. Hata hivyo, EP hiyo haikupokelewa kwa ukubwa kama ilivyotarajiwa, na imeonekana kuwa bado mashabiki wengi wanamchukulia zaidi kama mchekeshaji kuliko mwimbaji. Pamoja na hilo, juhudi zake zinaonesha ujasiri wa kujaribu na kupanua wigo wa vipaji vyake.

JANY BOY / GASPER

JANY BOY na GASPER – Marafiki Wawili Wenye Ndoto Moja

JANY BOY na GASPER ni marafiki wa karibu sana, wasanii, waimbaji na watunzi wa muziki wanaofanya kazi kwa kushirikiana. Wanatambulika zaidi kupitia mtindo wao wa Afrobeat, ambao umepokelewa kwa upendo mkubwa tangu mwaka 2024.

Hadi sasa mwaka 2026, wawili hawa bado wanaendelea kufanya vizuri, wakizidi kukua na kujijengea jina kubwa kwenye tasnia ya muziki. Wamekuwa mfano wa wasanii wa Kimbembe wenye ndoto, nidhamu na malengo makubwa ya kufika mbali kimataifa kupitia muziki

GASPER / ILUSTAR / JANY BOY

Tukio la Phoenix, Arizona – Afrobembe Yazidi Kupaa

Mnamo tarehe 24 Januari 2026, ILUSTAR, JANY BOY na GASPER walialikwa pamoja kwenda Phoenix, Arizona. Katika safari hiyo, walipata fursa ya kukaa hotelini pamoja na LUCCIE BABY, dancer maarufu na mrembo aliyewavutia mashabiki wengi.

Wakiwa pamoja, walirekodi na kucheza baadhi ya clip za kuchekesha na za burudani, bila vurugu wala drama, jambo lililopendwa sana na mashabiki wao. Tukio hilo liliibua mazungumzo mengi mitandaoni, ambapo watu wengi walianza kusema wazi kuwa muziki wa Afrobembe umeanza kukua kwa kasi.

Ndoto ya “EBEMBE TO THE WORLD” sasa imeanza kuonekana wazi, na wasanii hawa watatu wamekuwa sehemu muhimu ya safari hiyo ya kihistoria.

Imeandikwa na:

Omari Juma

@omriamajl

Posted in