Omriama is an online media platform delivering entertainment, music, business, and international news from Tanzania and around the world.

Tukio la Fumanizi Hotelini Kentucky Lasababisha Mjadala Mkubwa Mitandaoni
JULLY ALIVYO KAMATWA NA POLISI

Jana, tarehe 27 Januari 2026, mitandao ya kijamii ilisambaza kwa kasi kubwa video kadhaa zikionyesha tukio la wanandoa wawili waliodaiwa kufumaniana ndani ya hoteli moja jimboni Kentucky, Marekani. Video hizo zilisababisha mjadala mpana miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, hasa kutokana na mazingira na maelezo yaliyoambatana na tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa, mwanaume anayehusishwa na tukio hilo ni raia wa asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambaye awali aliwasili Marekani kupitia mpango wa hifadhi (green card). Inadaiwa kuwa ameishi nchini humo kwa muda sasa, akiwa jimboni Kentucky pamoja na mke wake.

Taarifa zinaeleza kuwa siku ya tukio, mwanaume huyo alipokea taarifa kutoka kwa watu wa karibu kwamba mke wake, anayejulikana kwa jina la Jully ni Mbembe pia, alikuwa ameonekana akiingia hotelini akiwa na mwanaume mwingine. Baada ya kupokea taarifa hizo, mwanaume huyo aliwahi kufika eneo la tukio usiku huo, ambapo alidai kumkuta mke wake akiwa chumbani pamoja na mwanaume mwingine, hali iliyoibua mgogoro mkubwa.

Zaidi ya hayo, madai yanaeleza kuwa tukio hilo halikuwa la mara ya kwanza, bali limekuwa likijirudia mara kwa mara, ikidaiwa kuwa wawili hao walikuwa wakikutana hotelini hapo kwa muda mrefu, hata kufikia madai ya kukutana karibu kila wiki.

Kutokana na hali kuwa tete, askari wa polisi waliitwa kufika eneo la tukio. Hata hivyo, changamoto kubwa ilijitokeza pale ilipobainika kuwa wahusika wakuu wa tukio hilo hawakuwa na uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiingereza, jambo lililolazimu polisi kutumia tafsiri kupitia simu ili kupata maelezo ya awali

VIDEO

Hadi sasa, utambulisho wa mwanaume aliyekutwa hotelini na mwanamke huyo bado haujawekwa wazi rasmi.

Kilichozidi kuchochea mjadala mitandaoni ni maoni ya watumiaji wengi waliomshambulia mwanaume aliyefumania, wakidai alishindwa kujieleza ipasavyo mbele ya polisi kutokana na changamoto ya lugha. Wengine walidai kuwa endapo angekuwa na uwezo mzuri wa kuzungumza Kiingereza, huenda angeweza kueleza kwa kina kilichotokea na hatua za kisheria zingechukuliwa mapema.

Kwa upande mwingine, sauti inayosikika kwenye baadhi ya video inadaiwa kuwa ni ya mwanamke huyo, akisema kuwa mume wake ndiye chanzo cha matatizo ya ndoa yao, akimtuhumu kwa tabia ya kutembea na wanawake wadogo, hali iliyomfanya naye kulipiza kisasi kwa kuingia kwenye mahusiano na wanaume wengine.

Tukio hili limeibua mjadala mpana kuhusu changamoto za lugha kwa wahamiaji, athari zake katika masuala ya kisheria, pamoja na changamoto za ndoa na maadili katika jamii za wahamiaji wanaoishi nje ya nchi zao.

@omriamajl

Posted in