Omriama is an online media platform delivering entertainment, music, business, and international news from Tanzania and around the world.

MZEE WILSON SELEHE AKUTWA AMEFARIKI KWENYE MTO WA ASALA KAMBINI NYARUGUSU

MTONI

Kwa masikitiko makubwa, tunawatangazia ndugu, jamaa na marafiki kifo cha mzee wetu mpendwa,

marehemu #WILSON_SALEHE, baba wa Deborah,

aliyekuwa mkazi wa Kijiji cha F2, CL1, PL19.

Marehemu amefariki dunia tarehe 09 Februari 2026, majira ya jioni saa kumi na mbili (6:00 PM), kufuatia ajali ya maporomoko ya maji yenye kasi kubwa katika mto unaojulikana kama #ASALA. Inaripotiwa kuwa marehemu alikuwa na miadi na marafiki zake katika kijiji cha MVUGWE. Baada ya mvua kukoma, aliaga mkewe na watoto wake na kuanza safari kuelekea MVUGWE.

Baada ya wasiwasi kutanda, familia kwa kushirikiana na vyombo vya usalama walifanya ufuatiliaji, ambapo ilibainika kuwa ndugu #WILSON_SALEHE hakuwa nasi tena duniani.

Msiba huu ni pigo kubwa kwa familia na jamii kwa ujumla. Marehemu alikuwa mshauri muhimu na mshiriki mkubwa katika masuala ya kifamilia na kijamii, na pengo lake halitazibika kwa urahisi.

Tunawaomba ndugu, jamaa na marafiki kushirikiana nasi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo hadi tutakapomfikisha marehemu katika makazi yake ya milele. Tunaomba pia faraja, dua na mshikamano wenu kwa msiba huu mzito uliotukuta.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa; jina la Bwana lihimidiwe.

@omriamajl

Posted in