Omriama is an online media platform delivering entertainment, music, business, and international news from Tanzania and around the world.

Kijana wa Kicongomani ARIO Afariki Dunia Nyarugusu, Kigoma

Kijana mmoja raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayefahamika kwa jina la ARIO, ambaye alikuwa mkimbizi na mkazi wa muda mrefu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu, mkoani Kigoma, amefariki dunia.

Marehemu ARIO, mkazi wa Kijiji cha R2, Zone ya Nne, Nyarugusu, inaripotiwa kuwa alifariki dunia tarehe 5 Februari 2026, wakati akiwa katika harakati za utafutaji wa maisha jijini Dar es Salaam.

ARIO aliwahi kuichezea timu za Fizi Raha na S2 Sport, na alikuwa anafahamika sana katika jamii ya wakazi wa Nyarugusu.

Marehemu anatarajiwa kuzikwa Jumapili, tarehe 8 Februari 2026.

Kwa mujibu wa taarifa za mtaani, chanzo cha kifo chake kinahusishwa na ajali mbaya ya gari aliyopata mwaka jana akiwa Dodoma, ajali iliyosababisha vifo vya watu kadhaa. Katika ajali hiyo, ARIO alipata majeraha makubwa yaliyosababisha mguu wake kukatika, na aliishi na jeraha hilo kwa muda, hali inayodaiwa kuchangia kifo chake.

Hata hivyo, taarifa nyingine zinaeleza kuwa marehemu alifariki Kigoma Mjini, ingawa chanzo rasmi cha kifo bado hakijathibitishwa.

Tutaendelea kuwajulisha pindi taarifa zaidi zitakapopatikana.

@omriamajl

Posted in