
Familia, ndugu, jamaa na marafiki wanataarifu kwa masikitiko makubwa kifo cha Luúndú Pierre (maarufu kama Thiago), kilichotokea siku ya Jumanne, tarehe 10 Februari 2026, katika Kijiji cha D3.2.1, Zone ya Tano, ndani ya Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma, Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa, marehemu alifariki dunia baada ya kujinyonga nyumbani kwake, tukio lililobainika baada ya mke wake kurejea nyumbani akitoka msibani. Tukio hilo liliwashtua ndugu, jamaa na jamii kwa ujumla.
Marehemu alikuwa mwimbaji wa kwaya katika Kanisa la Methodist Huru – Sekta ya Nne, na alitambulika kama mtu mwenye ushirikiano mzuri katika jamii na shughuli za kidini. Ameacha mke na watoto wawili, pamoja na familia, ndugu na marafiki wengi walioguswa na msiba huu mzito.
Msiba umewekwa nyumbani kwa marehemu katika Kijiji cha D3.2.1, Zone ya Tano, ndani ya Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, ambapo ndugu, jamaa na marafiki wanaendelea kutoa pole na kushiriki katika taratibu za mazishi.
🕊️ Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, na awape faraja, subira na nguvu familia, ndugu na wote walioguswa na msiba huu. Amina.
🇹🇿

