
Nyota wa Vinícius Júnior hatacheza mchezo wa mwisho wa LaLiga dhidi ya Athletic Club baada ya kupewa mapumziko maalum na klabu ya Real Madrid CF kuelekea majukumu ya timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia.
Taarifa zinaeleza kuwa Vinícius ameruhusiwa kuondoka mapema ili kujiunga moja kwa moja na kambi ya timu ya taifa ya Brazil itakayofanyika katika kituo cha mazoezi cha Granja Comary, karibu na Rio de Janeiro.
Msimu huu, Vinícius amemaliza akiwa na mabao 22 na pasi 10 za mabao katika michezo 53, licha ya Real Madrid kushindwa kutwaa taji kubwa lolote. Pia msimu wake uliandamwa na changamoto za uhusiano na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Xabi Alonso, kabla ya kiwango chake kuimarika baadaye.
Aidha, mustakabali wa Vinícius ndani ya Real Madrid bado unaendelea kuwa gumzo, huku mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya yakitajwa kusimama kwa sasa mpaka baada ya Kombe la Dunia.
Kupewa mapumziko mapema Vinícius kunaonyesha namna Real Madrid ilivyoamua kulinda nyota wake muhimu kuelekea mashindano makubwa ya kimataifa, hasa baada ya timu hiyo kukosa malengo muhimu mwishoni mwa msimu wa LaLiga.
Pia hali ya mkataba wake imeendelea kuvuta hisia kutokana na taarifa za tofauti zilizojitokeza kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya. Wachambuzi wa soka wanaamini kuwa Kombe la Dunia linaweza kuwa hatua muhimu itakayoongeza thamani na ushawishi wa Vinícius katika maamuzi yake ya baadaye ndani ya Santiago Bernabéu.
Cc @omriamajl
