We're open Closes at 5:00 pm

MUNGA ELOCHO, MWANAUME MWENYE UMRI WA MIAKA 22 KUTOKA CONGO, AKUTWA AMEFARIKI ROCHESTER

Polisi mjini Rochester, New York, wamemtambua mwanaume aliyekutwa amefariki katika eneo la karibu na Genesee River Trail mwishoni mwa wiki. Kwa mujibu wa Rochester Police Department, marehemu ametambuliwa kuwa ni Munga Elocho, mwenye umri wa miaka 22, ambaye anatokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Mwili wake ulipatikana Jumapili katika eneo lenye miti karibu na…

Polisi mjini Rochester, New York, wamemtambua mwanaume aliyekutwa amefariki katika eneo la karibu na Genesee River Trail mwishoni mwa wiki.

Kwa mujibu wa Rochester Police Department, marehemu ametambuliwa kuwa ni Munga Elocho, mwenye umri wa miaka 22, ambaye anatokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mwili wake ulipatikana Jumapili katika eneo lenye miti karibu na njia hiyo, kusini mwa daraja la Bausch Street, baada ya polisi kupata taarifa kuhusu uwepo wa mwili katika eneo la Vincent Street.

Munga elecho

Polisi wamesema kuna uwezekano kuwa Munga aliuawa katika eneo jingine na baadaye mwili wake ukapelekwa na kutupwa katika eneo ambako ulikutwa.

Hata hivyo, polisi bado hawajaweka wazi namna aliyofariki, huku uchunguzi ukiendelea kubaini ni lini na wapi aliuawa pamoja na mazingira yote yaliyozunguka kifo chake.

Wakati mwili huo ulipopatikana, Munga alikuwa amevaa T-shirt nyekundu yenye mistari myeupe na kaptula yenye rangi nyeusi.

Kitengo cha Major Crimes Homicide Unit cha Polisi wa Rochester kinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Cc @omarijumajl
Follow @omriamajltv @omriamajlnews @omriamajlsport
Company by www.omriama.com

Leave a Reply

Discover more from OMRIAMA

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading