Vilabu vikubwa vya Ulaya vinaendelea kufanya maandalizi ya kuimarisha vikosi vyao kuelekea msimu mpya, huku majina kadhaa makubwa yakitajwa katika tetesi za usajili zinazotikisa soko la wachezaji.
Taarifa zinaeleza kuwa Real Madrid imeonyesha nia ya kumfuatilia mshambuliaji wa Argentina, Julián Álvarez, huku pia ikihusishwa na kiungo wa Chelsea, Enzo Fernández. Hata hivyo, Chelsea inaelezwa kutokuwa tayari kumuachia nyota huyo kirahisi na inatajwa kuweka thamani kubwa kwa mchezaji huyo huku ikisisitiza kuwa bado ni sehemu muhimu ya mipango yao.

Wakati huo huo, Bayern Munich imeingia katika mbio za kuwania saini ya Marcus Rashford baada ya Barcelona kuonekana kusuasua katika mazungumzo ya kumleta mshambuliaji huyo wa Manchester United. Ripoti zinaeleza kuwa mshahara mkubwa wa Rashford unaweza kuwa changamoto katika kukamilika kwa dili hilo.

Majina mengine yanayotajwa katika tetesi za usajili ni pamoja na Gabriel Martinelli wa Arsenal, Ryan Gravenberch na Marc Cucurella, huku vilabu vikubwa vikionekana kuendelea kutafuta nyota watakaovisaidia kuongeza ushindani katika mashindano ya ndani na kimataifa.
@omriamajl

Leave a Reply