Usajili wa nyota wa NBA, Kawhi Leonard, kutoka Los Angeles Clippers kwenda Toronto Raptors umeahirishwa kwa muda wakati NBA ikiendelea na uchunguzi kuhusu madai ya ukiukwaji wa kanuni za matumizi ya fedha za mishahara ya wachezaji (salary cap) dhidi ya Clippers.
Timu hizo mbili zilifikia makubaliano ya uhamisho huo tarehe 30 Juni 2026, hatua ambayo ingemrejesha Kawhi Leonard katika klabu aliyoiongoza kutwaa ubingwa wa NBA mwaka 2019.
Hata hivyo, Toronto Raptors imesema haitakamilisha mchakato wa usajili hadi uchunguzi wa NBA utakapomalizika. Klabu hiyo imeeleza kuwa haitaki kubeba hatari endapo mkataba wa Leonard utabadilishwa au kufutwa kutokana na matokeo ya uchunguzi unaoendelea.
Kwa mujibu wa taarifa ya Raptors, ofisi ya NBA iliifahamisha klabu hiyo kuwa iwapo usajili ungekamilishwa kabla ya uchunguzi kuisha, Raptors ndiyo ingebeba athari zozote ambazo zingeweza kujitokeza kutokana na uamuzi wa mwisho wa ligi.
Kwa sasa, mustakabali wa uhamisho wa Kawhi Leonard unasalia kusubiri uamuzi wa NBA kuhusu uchunguzi unaoendelea dhidi ya Los Angeles Clippers.

Leave a Reply