Mambo yanaendelea kubadilika nchini Marekani baada ya serikali ya Rais Donald Trump kutangaza mabadiliko mapya yanayohusu waombaji wa Green Card.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, baadhi ya watu waliopo Marekani kwa visa vya biashara, utalii pamoja na sababu nyingine za muda mfupi, watalazimika kurejea katika nchi zao kwanza kabla ya kuendelea na mchakato wa kupata Green Card.
Taarifa zinaeleza kuwa waombaji hao watapaswa kuonana na maafisa wa ubalozi wa Marekani katika nchi zao ndipo waanze tena rasmi mchakato wa kuomba vibali vya kuishi Marekani kwa kudumu.
Hatua hiyo imeendelea kuzua mjadala mkubwa mitandaoni huku wengi wakionesha wasiwasi kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kwa wahamiaji pamoja na watu wanaosubiri kukamilisha taratibu zao za uhamiaji nchini Marekani.
@omriamajl
