
Kocha maarufu José Mourinho ameendelea kuzua gumzo kubwa baada ya taarifa kudai kuwa tayari amefikia makubaliano ya kurejea kuifundisha Real Madrid.
Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, makubaliano kati ya Mourinho, uongozi wa Madrid pamoja na klabu ya Benfica tayari yamekamilika na kinachosubiriwa kwa sasa ni kukamilika kwa baadhi ya taratibu rasmi za mwisho.
Ripoti hizo zinaeleza kuwa Mourinho alikubaliana na viongozi wa Real Madrid takribani siku kadhaa zilizopita na tayari mazungumzo kuhusu usajili mpya yameanza kufanyika.
Inaelezwa kuwa kipaumbele kikubwa kwa sasa ni kuongeza mabeki wapya ili kuimarisha safu ya ulinzi ya klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Mpaka sasa hakuna tamko rasmi lililotolewa na Real Madrid wala Mourinho mwenyewe, lakini taarifa hizo zimeendelea kuwasha moto mkubwa kwa mashabiki wa soka duniani.
@omriamajl



