Timu ya Taifa ya Marekani imepata nguvu mpya kuelekea mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Ubelgiji baada ya FIFA kusimamisha adhabu ya mshambuliaji Folarin Balogun, hivyo kuruhusiwa kucheza mchezo huo muhimu.
Balogun alikuwa ameonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika mchezo dhidi ya Bosnia na Herzegovina, jambo ambalo kwa kawaida huambatana na adhabu ya kukosa mechi moja moja kwa moja.

Hata hivyo, Kamati ya Nidhamu ya FIFA imeamua kusimamisha adhabu hiyo, hatua inayomruhusu mshambuliaji huyo kurejea kikosini na kuipa Marekani nguvu kubwa katika mchezo dhidi ya Ubelgiji.
Uamuzi huo umewapa matumaini makubwa mashabiki wa Marekani, ambao wanategemea Balogun kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji huku timu hiyo ikisaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2026.
Cc @omarijuma
Follow @omriamajl and @omriamajlnewss
Visit www.omriama.com

Leave a Reply