Timu ya Taifa ya Belgium imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuifunga Marekani mabao 4-1 katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa mjini Seattle.
Belgium ilianza mchezo kwa kasi na kupata bao la mapema kupitia Charles De Ketelaere baada ya safu ya ulinzi ya Marekani kufanya makosa. Marekani ilisawazisha kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na Malik Tillman, lakini furaha hiyo haikudumu kwa muda mrefu.
De Ketelaere alirejea tena kambani na kufunga bao la pili, huku Belgium ikiendelea kutawala mchezo kwa kiwango cha juu. Katika kipindi cha pili, Belgium iliongeza mabao mengine mawili na kuhitimisha mchezo kwa ushindi wa mabao 4-1.

Mshambuliaji Folarin Balogun, ambaye aliruhusiwa kucheza baada ya FIFA kusimamisha adhabu yake ya kadi nyekundu, alishindwa kuisaidia Marekani kubadili matokeo.
Kwa ushindi huo, Belgium imefuzu hatua ya robo fainali, huku safari ya Marekani katika Kombe la Dunia 2026 ikifikia tamati mbele ya mashabiki wake.
Cc @omarijuma
Follow @omriamajl and @omriamajlnews
Visit www.omriama.com

Leave a Reply